Back to top

Maambukizi ya Corona Kenya yafikia 3,860.

16 June 2020
Share

Idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona nchini Kenya imeongezeka na kufikia watu 3,860 hii ni baada ya maambukizi mapya 133 kuthibitishwa katika muda wa saa 24 zilizopita baada ya sampuli 3,255 kuchunguzwa.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amedokeza kuwa maambukizi hayo ni pamoja na 86 jijini Nairobi na 27 kaunti ya Mombasa.

Aidha idadi ya waliopona imefikia 1, 326 baada ya wagonjwa 40 zaidi kupona na kuruhusiwa kuondoka hospitalini.

Idadi ya waliofariki  kutokana na ugonjwa wa COVID 19 nchini Kenya imefikia 105 baada ya mtu mmoja zaidi kupoteza maisha.