Back to top

Maamuzi kesi ya Sabaya mpaka Oktoba 15.

01 October 2021
Share

Hukumu ya kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha namba 105 inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya, na wenzake wawili iliyotakiwa itolewe leo na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imeahirishwa mpaka Oktoba 15.

Maamuzi hayo yametolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Arusha Amalia Mushi kutokana na maandalizi ya maamuzi kutokukamilika.