Back to top

MAANDALIZI KUANZA KUTUMIKA SHERIA BIMA YA AFYA KWA WOTE

03 April 2024
Share


Naibu Waziri wa Afya, Mhe.Godwin Mollel amesema serikali imeanza maandalizi ya kuanza kutumika kwa sheria ya bima ya afya kwa wote ambapo kwa mujibu wa kifungu cha kwanza cha sheria ya bima ya afya kwa wote Waziri anaweza kuteua baadhi ya vifungu kuanza kutumika.

Akizungumza Bungeni Mhe.Mollel amesema baadhi ya vifungu ambavyo vinaweka mifumo imara ya kutekeleza bima ya afya kwa wote vimeshaainishwa na kuwasilishwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na sheria itatangazwa kuanza kutumika kabla ya mwisho wa mwezi huu kwa tarehe itakayotajwa.

Sheria ya bima ya afya kwa wote ilipitishwa na bunge tarehe moja Novemba mwaka 2023 na Mhe.Rais ameidhinisha Sheria hiyo tarehe 19 Novemba 2023 huku ikichapishwa katika gazeti la serikali la tarehe moja Disemba 2023.