
Ikiwa ni siku ya tatu ya maandamano mfululizo yaliyoitishwa na Upinzani nchini Kenya, kwa lengo la kupinga gharama kubwa za maisha, Mfanyabiashara ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wazalishaji Kenya (Kenya Association of Manufacturers), Rajan Shah, amesema nchi hiyo inapoteza zaidi ya Ksh. Bil. 2 (sawa na Bil. 34.4 za kitanzania) kila siku, kutokana na maandamano hayo.
