Back to top

MABADILIKO YA TABIANCHI YAATHIRI UTOAJI FEDHA

18 April 2024
Share

Waziri wa Fedha, Mhe.Dkt.Mwigulu Nchemba amesema utekelezaji wa bajeti Kuu ya Serikali unaathiriwa na hali mbaya ya hewa inayosababishwa na mabadiliko ya tabianchi.

Akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika wa Shirika la Fedha la Kimataifa, Bwana Willie Nakunyada Jijini Washington, Marekani ,amesema kiasi kikubwa cha fedha ambacho kingetumika katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi, kinaelekezwa katika kukabiliana na athari za mafuriko.

Amesema wakati wa utekelezaji wa bajeti inayoendelea ya mwaka 2023/2024, mabadiliko ya tabianchi yameathiri mtiririko wa utoaji wa fedha kwenda kwenye miradi ambayo ingesaidia kuchachua shughuli za kiuchumi badala yake zinatumika krekebisha miundombinu iliyoharibuwa na mafuriko ikiwemo madaraja, barabara na miundombinu mingine ya huduma za jamii.

Ametoa rai kwa washirika wa Maendeleo likiwemo Shirika la Fedha la Kimataifa kusanamna ya kusaidia bajeti ya Serikali ili kukabiliana na majanga hayo pamoja na kufanikisha mipango ya serikali ya kuimarIsha uchumi wake na kuhudumia wananchi.