
Mabalozi wanaowakilisha nchi mbalimbali hapa nchini Tanzania, wametembelea Hospitali ya Benjamin Mkapa kujionea huduma zinazotolewa.
Mabalozi hao walioongozwa na Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Mahmoud Thabit Kombo pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Rosemary Senyamule, kuitembelea Hospitali wamejionea huduma mbalimbali ikiwemo Idara ya Magonjwa ya Dharura na wodi maalumu za viongozi.
Kwaupande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Kessy Shija, amesema BMH ipo na wataalam wa viwango vya juu na inatoa huduma za matibabu ya kibingwa na bingwa bobezi na ipo tayari kuwa hudumia mabolozi watakapo hamia hapa Dodoma.
"BMH ina wataalam waliobobea katika maeneo mbalimbali, wataam waliobobea katika magonjwa ya dharua, figo, moyo, ubongo, upasuaji wa matundu madogo, wanawake, njia ya mkojo, watoto na magonjwa mengine mbalimbali, tupo tayari kuwahudumia kwa viwango vya juu kabisa" Amesema Dkt. Shija.
Dkt.Shija ameongeza kwa kuwashukuru Waziri Mahmoud Thabit Kombo na Mkuu wa Mkoa Mhe. Rosemary Senyamule kwa kuongoza ziara hiyo ya mabalozi kutembelea BMH.
"Namshukuru Mhe. Waziri Kombo na Mkuu wa Mkoa Senyamule kwa kuongoza ziara ya mabalozi kuweza kuitangaza Dodoma kupitia hospitali yetu ya Benjamin Mkapa kujionea huduma za ubingwa wa juu zinazotolewa"Amesema Dkt. Shija.