Back to top

Mabula akemea ucheleweshaji na utoaji Hati za Ardhi.

14 August 2019
Share

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula amekemea ucheleweshaji na utoaji Hati za Ardhi katika Manispaa ya Halmashauri ya Tabora mkoani Tabora na kueleza kuwa hali hiyo inachangia kuikosesha serikali mapato yatokanayo na kodi ya ardhi.

Dkt.Mabula ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi pamoja na kukagua mifumo ya kodi kwa njia ya kielektroniki na Masijala ya ardhi katika mkoa wa Tabora.