Back to top

MABULA AMSHUKURU RAIS SAMIA KWA PESA ZA PROGRAMU YA UPIMAJI ARDHI

14 September 2022
Share

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Dkt Angeline Mabula, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa  kuiwezesha wizara yake kupata fedha kiasi cha Shilingi Bilioni 50 kwa ajili ya programu ya kupanga, kupima na kumilikisha ardhi nchini.

Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango iliipatia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi shilingi bilioni 50 kwa ajili ya kuzikopesha Halmashauri 55 kutekeleza Programu ya Kupanga, Kupima na Kumilikisha Ardhi nchini. 

Alisema, utolewaji wa kiasi hicho cha fedha kumewezesha mkoa wa Mwanza kupatiwa shilingi Bilioni 6.691 zilizosaidia kutekeleza miradi ya kupanga, kupima na  kumilikisha ardhi katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo. 

Dkt.Mabula ametoa shukrani hizo, mbele ya Makamu wa Rais Mhe. Dkt Phillip Isdori Mpango wakati wa uzinduzi wa stendi mpya na ya kisasa ya mabasi na maegesho ya malori iliyopo eneo la  Nyamhongolo wilayani Ilemela.