Back to top

MABULA ASIKILIZA KILIO CHA WALIOKUWA WAFANYAKAZI TPL

03 August 2023
Share


Serikali imesikiliza kilio cha waliokuwa wafanyakazi katika shamba la Tanzania Plantation, lilipo Wilaya za Arusha na Arumeru mkoa wa Arusha kwa kuwapatia maeneo kwa ajili ya kujenga makazi, kilimo pamoja na ufugaji.

Akizungumza na wananchi wa kitongoji cha Lucy eneo la Bwawani wilayani Arumeru mkaoni Arusha, Dkt Mabula amesema, kutokana na uaminifu waliokuwa nao wananchi hao kwa muda mrefu, katika eneo hilo kwa kuendelea kutunza mashamba hata pale wawekezaji walipotetereka,  serikali inakwenda kuwapatia maeneo ya kujenga nyumba zao za makazi na kumilikishwa kisheria.

Dkt.Mabula ameongeza kuwa kama hiyo haitoshi Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kutambua kuwa wananchi hao bado ni wakulima na wana nguvu za kufanya shughuli za kilimo, ameelekeza pamoja na kupatiwa eneo la ujenzi wa nyumba wapatiwe pia walau ekari mbili kwa ajili ya shughuli za kilimo.