Back to top

MABULA ATAKA MPANGO WA MATUMIZI YA ARDHI, MRADI WA MAJI BUTIMBA

15 September 2022
Share


Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula ametoa wito kwa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) kuweka mpango wa matumizi ya ardhi katika eneo la Mradi wa wa Chanzo na Kituo cha Tiba ya Maji cha Butimba mkoani Mwanza.

Dkt.Mabula ametoa wito huo, wakati wa uwekaji jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa chanzo na kituo cha tiba ya Maji Butimba jijini Mwanza uliofanywa na Makamu wa Rais Dkt Phillip Isdori Mpango.

Ameishukuru MWAUWASA kwa kuweka uzio katika eneo linalozunguka mradi huo na kueleza kuwa, eneo hilo likiachwa wazi watu wataingia na ndipo migogoro ya ardhi inapoanza na kusisitiza kuwa mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza imefanya jambo zuri la kuweka uzio.

Hata hivyo, amesema pamoja na hatua ya kuwekwa uzio iliyofanywa na mamlaka hiyo lakini mpango wa matumizi bora ya ardhi kwenye eneo hilo ni muhimu ili kujua mahitaji ya huduma mbalimbali.