
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewataka Makamishna wa Ardhi Wasaidizi wa mikoa nane nchini kujitathimi kutokana na kushindwa kutoa taarifa ya uhakiki wa mashamba katika muda uliopangwa.
Dkt Mabula ametoa kauli hiyo wakati wa kikao kazi cha Makamishna wa ardhi wasaidizi wa mikoa 26 nchini kilichofanyika mkoani Dar es Salaaam.
Makimishna wa Ardhi Wasaidizi wanaotakiwa kujitathmini ni kutoka mikoa ya Arusha, Dodoma, Geita, Kagera, Njombe, Shinyanga, Simiyu na Songwe. Hadi wakati Dkt Mabula anakutana na Makamishna ni mikoa 17 pekee iliyowasilisha taarifa za uhakiki wa mashamba
Aidha, Waziri wa Ardhi ameonesha kutoridhishwa na utendaji kazi wa Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Wizarani Bw.Venance Mworo na kuelekeza Mkurugenzi huyo kuhamishwa Wizarani kutokana na kushindwa kwenda na kasi ya ubadilishaji mifumo ya TEHAMA hasa ikizingatiwa wizara kwa sasa iko katika mabadiliko makubwa ya kwenda katika mifumo ya kidigitali.
