Back to top

Machinga Arusha wapewa vitambulisho ili wafanye biashara kwa uhuru.

16 May 2018
Share

Mamlaka ya Mapato Tanzania imetoa vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo wa mkoa wa Arusha ikiwa ni sehemu ya kuwawezesha kufanya biashara zao kwa uhuru na kuweza kulipa kodi bila usumbufu. 

Akizungumza wakati wa utoaji wa vitambulisho hivyo Mkuu wa wilaya ya Arusha Bw Fabian Dakaro amesema hatua hiyo itatoa fursa ya  kuwatambua na kuwasaidia kuboresha biashara zao.

Kwa upande wake Kamshina Mkuu wa TRA Bw Abdul Zuberi amewataka wafanyabiasha hao kutumia fursa hiyo vizuri na kuheshimu  sheria.

Baadhi ya wafanyabiashara wameishikuru tra kwa kuwajali na wamewaomba wadau wengine kuendelea kuwasaidia.