Back to top

Macron amteua Jean Castex kuwa Waziri Mkuu mpya Ufaransa.

04 July 2020
Share

PARIS.

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron amemteua Jean Castex kuwa Waziri Mkuu mpya, kama sehemu ya kuifanyia mabadiliko serikali yake.

Ikulu ya Ufaransa, Elysee imesema kuwa Castex, mwenye umri wa miaka 55, amekuwa akiongoza mkakati wa Ufaransa wa kupunguza hatua za kuzuia kusambaa kwa virusi vya Corona.

Jean Castex kuwa Waziri Mkuu mpya -Ufaransa.

Uteuzi wa Castex, ambaye ni mtumishi wa umma umefanyika saa chache baada ya Edouard Philippe pamoja na serikali yake yote kutangaza kujiuzulu mapema jana.

Macron anafanya mabadiliko ya serikali ili kuangazia zaidi katika kuufufua uchumi wa nchi hiyo baada ya miezi kadhaa ya kuwepo kwa vizuizi vilivyowekwa ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya Corona.

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron

Macron amemuagiza Castex kuunda serikali na Baraza la mawaziri la Ufaransa linatarajiwa kutangazwa ifikapo Jumatano ijayo.