Back to top

Madaktari feki wa mifugo mbaroni, wafugaji watahadharishwa.

15 December 2019
Share

Idara ya mifugo jijini la Tanga inawashikilia madaktari  wawili  waliokuwa  wakitoa chanjo ya ugonjwa homa ya mapafu kwa ng'ombe bila kusajiliwa na baraza la mifugo nchini.

Vijana hao Raphael Shesaa na Evance Mushi wamekutwa wakiwa na wateja ndipo wataalam wa mifugo kutoka halmashauri ya jiji la Tanga walipobaini kuwa watuhumiwa hao hawana usajili unaowawezesha kufanya kazi ya kutibu na kutoa chanjo kwa mifugo.

Dk,Kisaka amewahadharisha wafugaji kuhakikisha kuwa wanatumia madaktari waliokuwa na usajili la sivyo mifugo yao inaweza kuathirika.