
Shirika la madaktari wasio na mipaka limesema, msafara wa timu ya madaktari katika Mji Mkuu wa Sudan, Khartoum, umeshambuliwa na watu wenye silaha, kisha kuwachapa viboko madaktari waliokuwa kwenye msafara huo.
.
Timu hiyo ilikuwa ikipeleka vifaa kwenye hospitali za kusini mwa Khartoum ambapo pia gari lao moja limeibiwa na watu hao.