Back to top

Madereva 50 wanaosafirisha mafuta kutoka Dar mpaka Rwanda wagoma.

31 March 2018
Share

Madereva wa malori 50 wanaofanya kazi ya kusafirisha matenki ya mafuta ya petroli na diseli kutoka jijini Dar es Salaam kwenda Rwanda, kwa mara nyingine wamegoma kupakua mafuta waliyopeleka nchini Rwanda, kwa madai kuwa, kipimo kinachopima mafuta yao si-rafiki kwao.

Madereva hao wamesema hii siyo mara ya kwanza wanalazimishwa wapime mafuta waliyoleta nchini humo kwa kutumia kipimo kinachowakata mafuta, kwani tukio hili limekuwa likijirudia, yapata miaka miwili sasa na safari hii wamesema hawakubali.

Huku madereva hao wakilalamikia kipimo hicho ambacho wanadai si rafiki kwao, kampuni iliyoagiza mafuta hayo pamoja na shirika la viwango nchini Rwanda RSB, wanadai kuwa kipimo hicho hakina kasoro hata moja bali madereva hao wamekuwa na tabia ya kuchota mafuta pindi wawapo njiani kuja nchini humu. Huyu hapa ni Maurice Charles anayehusika na kitengo cha upimaji katika shirika la viwango nchini Rwanda RSB.

Ili kujua ukweli wa swala hilo, kampuni iliyoagiza mafuta hayo imelazimika kuchukua tenki lililokuwa tupu na kulipakia mafuta yanayolingana na lita elfu 36 kisha wakapima na kukuta upungufu wa lita mia tatu za mafuta na kutokana na tatizo hilo, kampuni hiyo imetangaza kupunguza uagizaji mafuta kupitia Tanzania kwa kile inachodai inaepuka hasara.