Kamanda wa polisi wa wilaya ya Mbinga SSP Ramia Mganga amewataka madereva bodaboda wilayani humo kufuata sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuzuilika kwa kufuata sheria.
Pamoja na wito huo kwa waendesha bodaboda SSP Ramia Mganga pia amewataka maofisa elimu Kata waliokabidhiwa pikipiki na serikali hivi karibuni kufuata sheria na kutozitumia pikipiki hizo kufanyia biashara na kwamba watapokiuka sheria hatua zitachukuliwa dhidi yao.
Wakati huo huo mfuko wa taifa wa bima ya afya NHIF nao unawaasa waendesha boda boda kujiunga nao ili kutibiwa kwa gharama nafuu pindi wanapopata ajali.