
Madereva wa daladala, mkoani Arusha wamegoma kutoa huduma, kwa muda usiojulikana, kuanzia leo Agosti 14, 2023, wakilalamikia viongozi wanaosimamia usafirishaji mkoani humo kufumbia macho suala la pikipiki zenye magurudumu matatu maarufu kama Bajaj kufanya kazi sawa na daladala, ikiwa ni tofauti na leseni ya pikipiki hizo.
.
Wakizungumza na ITV madereva hao wamesema mnamo Julai 03, 2023, walisitisha kutoa huduma hiyo, lakini viongozi wa Mkoa na Wilaya walifika na kuzungumza nao, na kuwaahidi kuwa wanalifanyia na kwamba litakwisha, hali ambayo wamedai imekuwa kinyume na imewasababishia uhasama mkubwa kati yao na madereva wa Bajaj.
