
Kamanda wa Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha Solomon Mwangamilo amesema kuanzia sasa watawachukulia hatua za kisheria madereva wa magari ya serikali wanaotumia kivuli cha kuwaendesha viongozi wa serikali kuvunja sheria za usalama barabarani na kusababisha ajali mara kwa mara ambapo pia amesisitiza kuwa watawachukulia hatua hata pale watakapokuwa na wanaowaendesha.
