Back to top

MADEREVA ZAIDI YA 930 WAKAMATWA SHINYANGA

26 May 2023
Share

Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga, limewakamata madereva zaidi ya 930 kwa makosa hatarishi ,ikiwemo kuendesha mwendo kasi, huku madereva 11 wa mabasi ya kubeba abiria kutoka kwenye makampuni mbalimbali wakifikishwa mahakamani kwa kosa hilo.
.
Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Jeshi hilo mkoani humo, ACP Janeth Magimi , pia amebainisha kuwa wizi wa mafuta ya dizeli katika kujenzi wa reli ya kisasa ya SGR umepungua, kufuatia oparesheni na misako mbalimbali inayoendelea.