Back to top

ZUMARIDI AHUKUMIWA MWAKA MMOJA JELA

25 January 2023
Share

Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mwanza imemuhukumu Mchungaji Diana Bundala, maarufu kama Mfalme Zumaridi, kifungo cha mwaka mmoja jela na wenzake 4, baada ya kukutwa na hatia katika makosa mawili kati ya matatu yaliyokuwa yakimkabili yeye pamoja na washtakiwa wengine 8 ambapo wanne kati yao wameachiwa huru baada ya kukutwa hawana hatia.
.
Hata hivyo, Katika hukumu hiyo, Mfalme Zumaridi atatumikia kifungo hicho, kwa mwezi mmoja katika gereza la Butimba lililopo jijini Mwanza, baada ya kuondolewa kwa muda miezi 11 aliyokaa mahabusu.