Back to top

Mafuriko yaziba barabara kuu ya Songea-Tunduru-Dar es salaam.

10 January 2020
Share

Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali mkoani Ruvuma, zimesababisha mafuriko katika daraja la mto Luhila mjini Songea na kuziba kwa muda wa zaidi ya saa nne barabara kuu ya Songea-Tunduru kwenda Mtwara na Dar es salaam.
 
ITV imeshuhudia baadhi ya watumiaji wa barabara hiyo wakikwama kwa muda wa zaidi ya saa nne kuvuka eneo hilo kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani humo.
 
Akizungumza na ITV, Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Bi. Christina Mndeme pamoja na kuahidi serikali kuendelea kuchukua hatua ya kujenga daraja litakalohimili uwingi wa maji katika eneo hilo, lakini pia anatoa tahadhari kwa wananchi kuacha kujaribu kuvuka madaraja na barabara zilizojaa maji.