Wafanyabiashara wa mafuta mkoani Njombe wamesema kuadimika kwa bidhaa hiyo kunatokana na kukosekana kwa malighafi katika viwanda vinavyozalisha na kupelekea bei ya mafuta kupanda na kuadimika katika baadhi ya maeneo.
Baadhi ya wafanyabiashara waliozungumzia hali ya biashara ya mafuta mjini Njombe wamesema kuwa licha bidhaa hiyo kupanda lakini pia inakabiliwa na chanagamoto ya mrundikano wa kodi.
Kwa upande walaji wa bidhaa hiyo wakiwemo wamiliki wa migahawa na hoteli wamesema kuwa kuadimika na kupanda kwa bei ya mafuta kunapelekea kupungua kwa wateja kutokana na bei za vyakula kupanda.