Back to top

Magaidi wawili wakamatwa Kenya

28 April 2022
Share

Jeshi la KDF nchini Kenya limewakamata watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni magaidi wa Al Shabaab katika eneo la Horbati mpakani mwa Kenya na Somalia wakisafirisha silaha kutoka Somalia hadi Kenya kwa kutumia pikipiki ambapo Jeshi hilo limebainisha kuwa silaha zilizokamatwa ni Bunduki 11 aina ya AK47 na Magazine 13.