Back to top

Magufuli amteua Humphrey Polepole kuwa Mbunge wa Bunge la Tanzania.

29 November 2020
Share

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli leo tarehe 29 Novemba, 2020 amefanya uteuzi wa Wabunge 2 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwanza, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Humphrey Polepole kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Bw. Humphrey Polepole ni Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Pili, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bi. Riziki Said Lulida kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wabunge Wateule hao wataapishwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.