Back to top

Magufuli ataka uhusiano wa kiuchumi nchi za Afrika, Nordic uimarishwe

08 November 2019
Share

Rais wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli amesema ni lazima kubadishwa muelekeo na kuingia kwenye uhusiano wa kisasa baina ya mataifa ambayo yanajikita kwenye ushirikiano wa kiuchumi kupitia biashara na uwekezaji, na diplomasia ya uchumi ndio iwe msingi wa uhusiano na ushirikiano baina ya mataifa hayo.

Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa pamoja wa ushirikiano wa baadhi ya nchi za Afrika na zile za  NORDIC, ambapo amezitaka nchi za bara la Afrika kuhakikisha zinanufaika na ushirikiano baina yao na nchi za NORDIC.

Amesema kwa bahati nzuri uwezo na fursa za kuingia kwenye ushirikiano madhubuti wa kiuchumi upo, ukizingatia nchi za Nordic ambazo ziko tano, Denmark, Firnland, Island, Norway na Sweden licha ya kuwa na eneo dogo la kilomita za mraba milioni 3.5 na idadi ya watu wapatao milioni 27 zina uchumi mkubwa.

"Tanzania ilikuwa Mwenyekiti wa ukombozi katika nchi za Afrika, hivyo harakati nyingi ziliendeshwa nchini kwetu ambapo kulikuwa na kambi nyingi za wapigania Uhuru"amesema rais Magufuli.

Mkutano huo umeshirikisha baadhi ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Barani Afrika na wawakilishi mbalimbali kutoka nchi za NORDIC.