Back to top

Magufuli kuongoza zoezi la kuagwa kwa Mkapa kabla ya kupelekwa Lupaso.

28 July 2020
Share

DAR ES SALAAM.


Rais John Magufuli leo anatarajiwa kuwaongoza viongozi wa ndani na nje ya nchi katika misa na kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu, marehemu Benjamin William Mkapa.

Shughuli hizo zinatarajiwa kuanza saa mbili asubuhi hii kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam ambako wananchi wamekuwa wakitoa hehima zao za mwisho kwa siku mbili.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jana  Msemaji Mkuu wa Serikali Dakta Hassan Abbas alisema Mawaziri, Manaibu Waziri wametakiwa kuacha magari yao kwenye viwanja vya Karemjee na watapelekwa uwanja wa taifa kwenye mabasi maalum.

Baada ya misa na kuuaga mwili wa marehemu Mkapa mwili utasafirishwa kwenda Kijijini kwao Lupaso kwa maziko.