Back to top

MAHAKAMA KUU DIVISHENI YA ARDHI YAPIGA HATUA USIKILIZAJI MASHAURI

20 July 2022
Share

Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi imepiga hatua kubwa ya usikikizaji mashauri ya ardhi katika kipindi cha kuanzia Julai 2021 hadi Julai 2022 na kusababisha kupungua kwa mlundikano wa mashauri kwenye Divisheni hiyo.

Ulinganishaji kiwango cha ukamilishaji mashauri unaonesha kuwa, Mahakama Kuu- Divisheni ya Ardhi imeweza kuboresha kasi ya kusikiliza mashauri na kuwa na mashauri 1,591 yaliyosikilizwa kuanzia januari 2022 sawa na asilimia 42% ya mashauri yanayoendelea kusikilizwa hadi kufikia mashauri 1,212 sawa na asilimia 48% ya jumla ya mashauri yaliyopo katika hatua ya kusikilizwa kwa taarifa ya hadi 11 Julai 2022.

Mwelekeo unaonesha kuwa, pamoja na kasi inayoendela ya usikilizwaji mashauri Mahakama Kuu- Divisheni ya Ardhi itabakiza asilimia 15% ya kesi ambazo hazijasikilizwa ifikapo mwisho wa mwaka 2022.

"Mahakama Kuu - Dvisheni ya Ardhi imeweza kupunguza mlundikano mashauri ya ardhi yaliyofunguliwa kuanzia Julai, 2021 hadi Julai, 2022 ambapo kwa Julai 2021 kulikuwa  na mashauri  359 yaliyosikilizwa’’Amesema Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu- Divisheni ya Ardhi Mhe.Agnes Mgeyekwa.