Back to top

Mahakama mkaoni Manyara yamuhumuku miaka 20 dalali wa meno ya Tembo.

09 June 2021
Share

Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Manyara imemhukumu dalali wa biashara ya meno ya Tembo Bw.Bernard Masalu Mgalula (54) mkazi wa jiji la Dar es Salaam kutumikia kifungo cha miaka 20 baada ya kukiri kosa la kuhujumu uchumi kwa kukutwa na meno 13 ya Tembo yenye thamani ya shilingi 240 katika kijiji cha Mayomayoka kata ya magara wilayani babati alikokuwa.

Masalu anahukumiwa katika kizimba cha mahakama hiyo mbele ya hakimu mfawidhi mwandamizi wa Bw.Simon Kobelo baada ya kukiri kosa lake la kukutwa na meno hayo ambayo ni sawa na kuua tembo saba huku washitakiwa wengine watatu, Yanderson Masumbuko,Ramadhani Swalehe akiwemo mwanamke mmoja Bi.Mwajuma Athumani wanaohusishwa na shauri hilo.

Shauri hilo limeendelea kusikilizwa kwa siku mbili mfululizo kwenye mahakama hiyo kwa washtakiwa hao watatu ambapo kwa mujibu wa upande wa Jamhuri ukiongozwa na mwendesha mashtaka wa serkali Bw.Petro Ngasa alitoa ushahidi wake kwa kuieleza mahakama hiyo kuwa washtakiwa hao mnamo februari 25 mwaka huu majira ya saa 10 walikamatwa na askari wa wanyamapori wa halmashauri ya wilaya ya babati kwa kushirikiana na askari wa hifadhi ya taifa ya TANAPA baada ya kuwekewa mtego na kukutwa na meno 13.

Mbali na Hakimu Kolobelo kutoa nafasi kwa washtakiwa hao ambao hawakuwa na wakili kuuliza maswali na baadae shauri hilo kuahirishwa hadi juni 14 mwezi kwa ajili ya kusikiliza utetezi kwa upande wa washtakiwa wote watatu na kurejeshwa mahabusu kutokana na shauri hilo la kuhujumu uchumi.