Back to top

MAHAKAMA YA ICC YATOA HATI, KUMKAMATA PUTIN

17 March 2023
Share

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) imetoa hati ya kukamatwa kwa Rais wa Urusi Vladimir Putin, ikimtuhumu kufanya uhalifu wa kivita kwa kuwahamisha watoto na raia wengine wa Ukraine kwenda Urusi kinyume cha sheria ambapo imesema uhalifu huo ulifanyika nchini Ukraine kuanzia Februari 24, 2022 wakati Urusi ilipoanzisha uvamizi wake kamili nchini Ukraine.
.
Licha ya kibali hicho kutolewa, bado hakuna uwezekano wa kiongozi huyo kufikishwa mbele ya mahakama hiyo, kwa sababu mbalimbali ikiwemo ya mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kuwakamata washukiwa, lakini inaweza kutumia mamlaka za ndani ya nchi ambazo zimesaini makubaliano yaliyounda mahakama hiyo, ambayo pia Urusi sio mwanachama wa makubaliano hayo.