Back to top

Mahakama ya wilaya ya Iringa yashindwa kusikiliza Kesi ya Nondo.

14 May 2018
Share

Mahakama ya hakimu Mkazi wilaya ya Iringa imeshindwa kuendelea kusikiliza ushahidi wa mashahidi wawili kati ya watano wa kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Mtandao wa wanafunzi nchini Abdul Nondo baada ya mshitakiwa kuiandikia barua mahakama hiyo akitaka hakimu anayesikiliza kesi hiyo kujitoa kutokana na yeye kupoteza imani na hakimu huyo mheshimiwa John Mpitanjia.

Katika barua yake hiyo Nondo ametaja sababu tano ikiwemo madai ya hakimu huyo kukutana na mmoja wa mashahidi na kumuhoji kama anaendelea kuwasiliana na Nondo.

Sababu ya pili Nondo anadai kila kesi hiyo inapoletwa mahakamani RCO. wa Iringa amekuwa akionekana kukutana na hakimu Mpitanjia kabla na baada ya kesi hiyo huku sababu ya tatu ya mshitakiwa Nondo kimkataa Hakimu Mpitanjia ikiwa ni mahusiano na mawasiliano mazuri na upande wa Jamhuri huku akiwa hana mahusiano mazuri na upande wa mshitakiwa.