Back to top

Mahakama yaahirisha ushahidi wa shahidi wa pili kesi ya Sabaya.

20 July 2021
Share

Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imeahirisha kusikiliza ushahidi wa shahidi wa pili wa Jamhuri Numan Jasin (17) katika kesi ya uyang’anyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili.

Wakili Mkuu wa serikali Tumaini Kweka ameiomba mahakama hiyo kuahirisha kusikiliza shauri Hilo kwa kuwa shahidi ameshindwa Kufika  mahakamani kwa sababu za kiimani, kwa Imani yake yuko kwenye Ibada ya sala ya Eid Alhaj.

Usikillizaji wa ushahidi wa shahidi huyo wa pili upande wa Jamhuri utaendelea Tena Alhamisi ya Julai 22 mwaka huu.