Back to top

Mahakama yampatia dhamana Mwenyekiti wa Mtandao wa wanafunzi.

26 March 2018
Share

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa imempa dhamana Mwenyekiti wa Mtandao wa wanafunzi  Bwana ABDUL NONDO.

Mahakama hiyo imetoa dhamana kwa masharti ya wadhamini wawili ku tia  saini  dhamana ya  Shilingi  Milioni 5.

Mahakama hiyo imesema kumnyima dhamana  mtuhumiwa huyo ni kumnykima haki yake ya kusoma,   hivyo apewe dhamana ili siku ya kesi ahudhurie kesi na siku nyingine aendelee na masomo.

Kesi ya Bwana NONDO itatajwa tena tarehe 10 mwezi ujao.