Baadhi ya Mahakimu na Majaji katika ngazi mbalimbali za mahakama mkoani Mbeya, wamedaiwa kubuni njia mpya za kupokea rushwa, ikiwemo ya kutumia miamala ya simu zisizokuwa zao , ili kuficha utambulisho wao, pale wanapofuatiliwa na vyombo vya dola.
.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dkt.Rashid Chuachua, wakati akifungua maadhimisho ya Wiki ya Sheria katika mahakama kuu kanda ya Mbeya.