Back to top

Majaliwa aagiza wakurugenzi wa halmashauri kufufua madarasa ya MEMKWA.

09 June 2021
Share

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanafufua madarasa kwa ajili ya Mpango wa Elimu ya Msingi kwa walioikosa (MEMKWA) ili kusaidia kupunguza ongezeko la watu wazima wasiojua kusoma na kuandika.

Ametoa agizo hilo wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la Kuadhimisha Miaka 50 ya Elimu ya Watu Wazima Tanzania.

Aidha, amewataka watumie madarasa hayo kuwezesha watu wazima wapate stadi mbalimbali pamoja na stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK).

Waziri Mkuu amesema kuwa pamoja na kutekeleza majukumu mengine, Taasisi ya Elimu ya Watu wa Wazima iendelee kutekeleza kikamilifu jukumu lake la msingi la utoaji wa elimu ya watu wazima hadi katika ngazi ya wilaya.