Back to top

Majaliwa aridhishwa na ujenzi wa reli ya SGR Dar hadi Kilosa, Morogoro

12 September 2021
Share

Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa ameridhishwa na kiwango cha ujenzi wa reli ya kisasa ya (SGR) kutoka Dar es Salaam hadi Kilosa mkoani Morogoro ambapo kwa mara ya kwanza ametumia treni ya wahandisi kutoka Dar es Salaam hadi Kilosa ikiwa ni zaidi ya kilomita 245
.
Waziri Mkuu amesema serikali mpaka sasa imeshanunua mabehewa ya treni 12 ya kwanza ambapo yataingia nchini na kuanza matumizi mwenzi 12 kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro.
.
Mapema kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Bw.Martin Shigella amesema reli hiyo itakuja na frusa za kujenga uchumi wa nchi ambapo wanakusudia kujenga stendi kubwa ya mabasi katika stesheni kuu ya Morogoro baada ya kumalizika kwa mgogoro wa eneo uliokuwepo.