
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekagua ujenzi wa madarasa katika shule ya sekondari Babati iliyopo mkoani Manyara ambapo amemuagiza Mkuu wa Wilaya kusimamia maboresho ya madawati katika shule hiyo kwa kuweka mbao badala ya bati kama ilivyo sasa ili kuepusha madhara kwa watoto, bila kuathiri mwenendo wa masomo kwa wanafunzi.
