
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amefanya ziara ya kukagua soko la wazi la wafanyabiashara wadogo maarufu kama machinga lililopo jijini Dodoma huku akimtaka Mkandarasi wa ujenzi wa soko hilo Mohammed Builders kumaliza ujenzi wa soko hilo kwa wakati.

Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa Soko la Wafanyabiashara Wadogo (Machinga Complex) lililoko barabara ya Bahi Mkoani Dodoma na kusema ameridhishwa na ujenzi wa soko hilo ambapo amewataka wafanyabiashara wadogo wa mkoa huo wafuate utaratibu utakaowekwa na mkoa huo mara baada ya ujenzi kukamilika.
Waziri Mkuu ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Dodoma kwa ubunifu na kuwataka viongozi hao waendelee kusimamia mradi huo na kuukamilisha kwa wakati pamoja na kubuni maeneo mengine ya nje ya mji Ili kukuza maeneo mengi zaidi kibiashara katika mkoa huo.

Kwa upande wake, Waziri wa (TAMISEMI), Innocent Bashungwa amesema Mkoa wa Dodoma umefanya kazi kubwa ya kutekeleza mradi rafiki kwa wamachinga wa mkoa huo. “Niwasihi wakuu wa mikoa mingine kuiga mfano huu kwa kujenga miradi ya kuwapanga machinga kulingana na mazingira yaliyo katika mikoa yenu.
