
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameondoka nchini kuelekea Qatar na Jordan kwa ziara ya kikazi na atamuwakilisha Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan katika vikao na viongozi wakuu wa nchi hizo ambapo Tanzania na Qatar zimepanga kuanzisha Tume ya Ushirikiano itakayosimamia masuala mbalimbali ya kiuchumi ikiwemo usafiri wa anga huku akiwa Jordan Waziri Mkuu atashiriki mkutano wa kujadili hali ya usalama katika eneo la Mashariki mwa Afrika hususan Msumbiji na maeneo jirani.
