Back to top

Majaliwa:Chanjo ya UVIKO-19 ipo nchini wenye nia wakachanje.

21 July 2021
Share

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema chanjo ya ugonjwa wa Corona ipo tayari nchini mwananchi yoyote anayetaka kuchanjwa akachanje kwa ajili ya kupata kinga dhidi ya ugonjwa huo.
 
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo  katika Baraza la Eid El Adha lililofanyika katika Msikiti wa Mtoro, Ilala jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwakumbusha na kuwasisitiza wananchi wote waendelee kuchukua hatua za kujikinga na ugonjwa wa UVICO-19.

Waziri Mkuu amesema ni vema kwa sasa wananchi wakajiepusha na mikusanyiko isiyokuwa ya lazima na wazingatie kukaa umbali wa mita moja au zaidi kutoka mtu mmoja hadi mwingine.
 
Amesema wananchi wanatakiwa wafanye mazoezi ya mara kwa mara kulingana na afya zao pamoja na mazingira yanayowazunguka, pia amewasihi wazingatie lishe bora.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu  Majaliwa ametoa rai kwa viongozi wa dini na waumini waendelee kuvumiliana, kustahamiliana na kushikamana katika kufanya ibada na kuienzi tunu ya amani.

 Kwa upande wake, Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Aboubakar Zubeir Bin Ally amewataka watanzania kuendelea kuimarisha maadili mema yatakayoisaidia nchi yetu.