Back to top

Majaliwa:Ikibainika mwendeshaji wa UDART anamatatizo ataondolewa.

10 May 2018
Share

Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa amesema serikali ikibaini muwekezaji wa mradi wa mabasi yanayoenda haraka jijini Dar es Salaam-UDART kuwa na matatizo itamuondoa haraka ili kupisha wawekezaji wengine wenye nia ya kuwekeza katika mradi huo.

Akizungumza wakati akijibu swali la Mbunge wa Kinondoni Mheshimiwa Maulid Mtulia aliyeuliza serikali imetenga fedha nyingi katika kuboresha mfumo wa usafiri hasa katika mabasi yanayoenda haraka katika jiji la Dar es Salaam, lakini bado mradi huo unachangamoto kati ya mwekezaji na Max-Malipo na hata miundombinu je serikali inampango gani kuboresha mradi huo.

Waziri Mkuu Mheshimiwa Majaliwa amesema serikali inaendelea kutafuta mwekezaji mwengine katika awamu ya pili ya mradi huo ili kuhamasisha ushindani zaidi na kusisitiza inapobainika mwendeshaji wa sasa anamatatizo yaliyokithiri serikali itamuondoa katika kazi hiyo.

Amesema serikali inaendelea kuondoa changamoto za mwendeshaji aliyeko sasa na kuanza kutafuta mwendeshaji mwingine ili kupata kampuni nyingine ambayo itaingiza mabasi yatakayowezesha kuimarisha sekta ya usafiri jijini dar es salaam.