Back to top

Majaliwa:Pasi zao za kusafiria zikamatwe hadi wamalize kazi.

07 May 2022
Share

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa ameagiza kukamatwa kwa pasi za kusafiria za wataalamu wa kampuni ya GAS Entec ya Korea Kusini wanaojenga meli ya MV Hapa Kazi Tu jijini Mwanza hadi wakamilishe kazi yao.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo wakati akizungumza na wananchi na viongozi wa mkoa huo mara baada ya kukagua ujenzi wa meli hiyo katika eneo la Mwanza South, wilaya ya Nyamagana, jijini Mwanza.

"Nimemwagiza Afisa Uhamiaji wa Mkoa akamate pasi zao mara moja na ahakikishe hakuna mtu anatoka nje ya mkoa huu hadi hii kazi ikamilike. Nimeambiwa wako saba, lakini hapa wako watatu. Watafuteni hao wengine wako wapi".Majaliwa

Wenye pasi hizo ni Mkurugenzi wa GAS Entek, Bw. Dong Myung Kwak, na wasaidizi wake Bw. Kyunghan Choi na Bw. Kyuh Yun Kwak ambaye ni mtoto wa Mkurugenzi huyo.