Back to top

Majambazi wateka basi na kuwapora mali abiria, mkoani Kigoma.

11 June 2021
Share

Watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wameliteka basi la abiria lenye namba za usajili  T 116 BHD mali ya kampuni ya Scorpion lililokuwa likitokea mkoani Shinyanga kuelekea Kasulu mkoani Kigoma na kisha kuwapora vitu mbalimbali abiria waliokuwa wakisafiri katika basi hilo.
.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo akiwa katika kituo kidogo cha polisi cha Makere, Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma Kamishna Msaidizi wa polisi James Manyama amesema tukio hilo limetokea katika pori lililopo jirani na kambi ya wakimbizi ya Nduta.

Aidha, katika tukio jingine Kamanda Manyama amesema jeshi hilo limeendelea na operesheni maalumu na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa mbalimbali pamoja na magunia 18 ya bangi yaliyokuwa yakitarajiwa kusafirishwa kuelekea nchi jirani ya Burundi.