Back to top

MAJAMBAZI WAWILI WAUAWA NA POLISI, KAGERA

23 January 2023
Share

Watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha za kivita, ikiwemo bunduki moja aina ya AK 47 iliyokuwa na magazini yenye risasi 25 na mabomu mawili ya kutupwa kwa mkono wameuawa na Jeshi la Polisi, wakati wakijiandaa kufanya matukio ya uhalifu katika maeneo yaliyopo wilayani Ngara mkoani Kagera, huku mmoja wao akifanikiwa kutoroka.