Back to top

MAJENGO YA DHARULA 128 YAJENGWA NDANI YA MWAKA MMOJA

17 September 2023
Share

Serikali imesema imejenga majengo ya huduma za dharura 128 na majengo ya Huduma za wagonjwa mahututi 78 ndani ya mwaka mmoja (2023), nchi nzima.
.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, katika ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, wakati akisalimia wananchi wa Wilaya ya Nanyumbu Mkoani Mtwara.
.
Aidha, Dkt. Mollel ameongeza kuwa ndani ya mwaka huu mmoja pia X-RAY za kisasa 199 zimenunuliwa na kusambazwa ambapo X-Ray moja ya kisasa inagharimu kiasi cha Tsh. Mil. 500/=.