Back to top

MAJENGO YA MAHAKAMA KUBORESHWA

03 November 2023
Share


Naibu waziri wa sheria na Katiba Mhe.Pauline Gekul, amesema serikali inaendelea kuboresha majengo ya Mahakama hapa nchini kwa kujenga majengo mapya na kuyakarabati zamani.

Naibu Waziri Gekul ameyasema hayo bungeni mkoani Dodoma wakati akijibu maswali yaliyoelekezwa kwa wizara hiyo.

Amesema majengo mengi yapo katika mpango wa kukarabatiwa katika mwaka huu wa fedha unaoendelea.

Mkutano wa kumi na tatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaendelea mkoani Dodoma.