Back to top

Maji yalitoka mwezi 1 tu baada ya kuzinduliwa - Wananchi Songea

17 October 2018
Share

Wananchi wa mitaa ya  Chandarua na Mitendewawa wilayani Songea mkoani Ruvuma  wamelalamikia mradi wa maji wa Chandarua kutotoa maji ambapo ulitoa maji kwa mwezi mmoja baada ya kuzinduliwa na mwenge na kisha kusimama huku wananchi wakipata shida kubwa ya maji.

Wananchi hao wametoa malalamiko hayo kupitia diwani wao wa kata ya Mshangano Bw. Rotary Mbawala ambaye amesema wananchi wake wanapata shida kubwa ya maji na kumuomba katibu tawala wa mkoa wa Ruvuma Profesa Riziki Shemdoe  kushughulikia tatizo hilo ambapo katibu huyo amemuagiza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Songea bw. Philipo Beno kushughulikia changamoto hiyo.