
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Bw.Amos Makalla amemkabidhi Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe, Geophrey Pinda, kitabu chenye malalamiko ya Ardhi yaliyoshughulikiwa na mkoa wake.
Makabidhiano ya kitabu hicho yamefanyika, katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, wakati wa ziara ya Mhe, Pinda kuzindua Kliniki ya Ardhi katika mkoa huo.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Mhe, Pinda amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa juhudi zake za kushughulikia migogoro ya ardhi na kuweka kumbukumbu za kero alizoshughulikia.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Amos Makala amesema, ni vizuri wizara ya ardhi pale inapokuta mkoa umefanya maamuzi kuhusiana na migogoro ya ardhi na wizara kupelekewa tena malalamiko basi ni vizuri ikarudi mkoa husika kuulizia ama kufanya mawasiliano kwa nia ya kutafuta njia nzuri ya kushughulikia mgogoro.
