Back to top

MAKALI MGAO WA UMEME KUPUNGUA MWEZI WA PILI

01 January 2024
Share

Rais wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan, amesema makali ya mgao wa umeme unaoendelea hapa nchini, utapungua mwezi wa pili mwaka huu wa 2024.

Amesema hilo litafanyika baada ya sehemu ya Nishati hiyo kutoka mradi wa uzalishaji umeme wa Mwawa la Mwalimu Nyerere utakapoingizwa kwenye gridi ya taifa.

Rais Samia amebainisha hayo wakati akitoa salamu za serikali kwa wananchi kwa mwaka unaomalizika wa 2023 kuelekea 2024.

Pia Rais Samia amewataka Watanzania kujiandaa na uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao utafanyika mwaka huu 2024.