Back to top

MAKAMBA AONGOZA KIKAO CHA MAWAZIRI 15 WA EAC

07 July 2024
Share

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb), ameongoza Mkutano wa faragha wa Mawaziri wa Mambo ya Nje na Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Afrika Mashariki katika Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika Zanzibar. 

Akizungumza katika Mkutano huo wa siku tatu ambao Mhe. Makamba Mhe. Makamba ni mwenyekiti, amesema Tanzania imejidhatiti kuhakikisha Jumuiya ya Afrika Mashariki inakuwa imara, yenye umoja na inayofikia malengo yake. 

“Madhumuni ya mkutano huu ni kuifanya familia yetu kuwa imara, kuifanya Jumuiya ya Afrika Mashariki kutekeleza majukumu yake vizuri, Tanzania kama moja ya waanzilishi wa Jumuiya hii tumejidhatiti kuona jumuiya ikiwa na umoja, imara na yenye kufanikiwa” Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Makamba